• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Johnson & Johnson ya Marekani yatangaza kusitisha jaribio la chanjo ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-13 18:58:09

    Kampuni ya Johnson & Johnson ya Marekani jana ilitangaza kuwa baada ya mtu aliyepatiwa chanjo kuwa na ugonjwa usioweza kuelezeka, hivyo kampuni hiyo inasitisha kwa muda jaribio la chanjo moja ya COVID-19.

    Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo inasema, kampuni hiyo itasitisha majaribio yote ya chanjo hiyo, likiwemo jaribio la kipindi cha tatu lililoanza mwishoni mwa mwezi Septemba. Hivi sasa kamati moja huru na wataalamu husika wa kampuni hiyo wanachunguza na kutathimini hali ya ugonjwa wa mtu huyu.

    Kampuni hiyo inasema, ugonjwa, ajali na matukio mengine mabaya ni hali inayoweza kutokea katika utafiti. Kampuni hiyo imeweka vigezo ili kuhakikisha kila ikitokea matukio mabaya inaweza kusitisha utafiti, na kuamua kama itaanza tena au la utafiti huo baada ya uchunguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako