• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka serikali ya Canada iondoe vikwazo vya maendeleo ya uhusiano kati yake na China

    (GMT+08:00) 2020-10-13 19:36:01

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo hapa Beijing amesema, serikali ya Canada inapaswa kuchukua hatua ya kurekebisha makosa, na kufanya bibi Meng Wanzhou arudi China kwa usalama, kuondoa vikwazo vya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Canada na kuufanya uhusiano huo urudi kwenye njia sahihi.

    Leo ni maadhimisho ya miaka 50 tangu China na Canada zianzishe uhusiano wa kibalozi. Bw. Zhao Lijian amesema katika miaka 50 iliyopita, kutokana na juhudi za China na Canada, uhusiano kati ya pande hizo mbili umepata maendeleo makubwa. Baada ya maambukizi ya virusi vya Corona kutokea, China na Canada ziliungana mkono na kusaidiana, na kushirikiana katika mapambano dhidi ya virusi hiyo.

    Amesema kuwa, Hivi sasa uhusiano kati ya China na Canada umekumbwa na taabu, chanzo ni kwamba Canada inamfunga mchina Bibi Meng Wanzhou asiyevunja sheria yoyote ya Canada kutokana na matakwa ya Marekani. China inaitaka serikali ya Canada kuchukua hatua kurekebisha makosa, na kufanya Bibi Meng arudi China kwa usalama, kuondoa vikwazo katika maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kuufanya uhusiano huo urudi kwenye njia sahihi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako