• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Somalia lawaua wanamgambo 11 wa kundi la al-Shabaab mkoani Lower Shabelle

    (GMT+08:00) 2020-10-13 19:36:09

    Takriban wanamgambo 11 wa kundi la al-Shabaab akiwemo kiongozi wao mwandamizi Abu Abdullahi Mustaf wameuawa jana Jumatatu na Jeshi la Taifa la Somalia SNA kwenye operesheni ya ulinzi wa usalama iliyofanyika katika mkoa wa Lower Shabelle.

    Kwa mujibu wa kamanda wa kikosi cha 143 cha SNA Ahmed Hassan Ziyad, operesheni ilianza baada ya jeshi kupokea taarifa za kiintelijensia kwamba wanamgambo wameanzisha jela za siri kwenye viunga vya mji wa Barrie hivyo jeshi likalenga eneo hilo. Amesema jeshi pia limewaachia huru wenyeji waliokuwa wanashikiliwa na wanamgambo kwenye jela hizo za siri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako