Waziri wa fedha wa Ghana Bw. Kenneth Ofori-Atta amehimiza uungaji mkono zaidi wa pande nyingi kwa ufufukaji wa uchumi wa Afrika baada ya janga la virusi vya Corona kumalizika.
Kwenye taarifa aliyotoa kabla ya kufanyika kwa mikutano ya majira ya mpukutiko ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Bw. Ofori-Atta ameomba Afrika iahirishiwe malipo ya madeni kwa muda wa miaka miwili na kupewa mkopo nafuu wa dola za kimarekani bilioni 300 ndani ya miaka mitatu ili kuharakisha ufufukaji wa uchumi wa bara hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |