Chuo kikuu cha Tsinghua, ambacho ni moja ya vyuo vikuu maarufu zaidi nchini China, kinatafuta ushirikiano wa kitaaluma na vyuo vikuu vya Afrika, ili kusaidia kuandaa raslimali watu kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo.
Naibu mkuu wa Chuo kikuu cha Tsinghua Yang Bin alisema hayo kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya video na Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah cha Ghana, ikiwa ni sehemu ya programu ya wiki ya uchumi na utamaduni kati ya Ghana na China. Yang amesema chuo kikuu cha Tsinghua kinatafuta kujenga muundo wa elimu ulio shirikishi na wenye ustahimilivu na washirika wake wa Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |