• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yajitahidi kuweka uwiano kwenye mfumo wa chakula

    (GMT+08:00) 2020-10-14 09:01:11

    Serikali ya Uganda imesema inajitahidi kuleta uwiano kwenye mifumo ya chakula ambayo imevurugika kutokana na athari za janga la virusi vya Corona vilivyoikumba dunia.

    Waziri wa Kilimo ameaambia wanahabari jijini Kampala kuwa, ingawa Uganda inazalisha chakula kinachotosha kulisha wananchi wake, lakini mifumo yake ya chakula bado haina uwiano. Amesema njaa, unene wa kupitiliza, uharibifu wa mazingira, upoteaji wa bioanuwai, upotevu na utupaji wa chakula na ukosefu wa usalama kwa wafanyakazi katika mnyororo wa chakula ni baadhi ya masuala yanayosababisha ukosefu wa uwiano.

    Wakati huohuo, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linatafuta dola za kimarekani milioni 15.3 ili kuwapatia chakula wakimbizi zaidi ya milioni 1.4 nchini Uganda. WFP imesema, wakimbizi hao wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula kutokana na kupungua kwa msaada wa chakula na vikwazo vinavyotokana na janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako