• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yakadiria uchumi wa dunia utapungua kwa asilimia 4.4 mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-10-14 09:01:30

    Ripoti ya Mustakabali wa Uchumi wa Dunia (WEO) iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imeonyesha kuwa, uchumi wa dunia utapungua kwa asilimia 4.4 kwa mwaka huu, ikiwa ni asilimia 0.8 zaidi ya makadirio yaliyotolewa mwezi Juni.

    Akizungumza na wanahabari kwa njia ya video wakati wa mkutano wa Kundi la Benki ya Dunia na IMF, Mchumi Mwandamizi wa Shirika hilo Gita Gopinath amesema ongezeko hilo linatokana na matokeo mazuri kiasi katika robo ya pili ya mwaka, na ishara za kufufuka kwa nguvu zaidi katika robo ya tatu ya mwaka.

    Ripoti hiyo imeonyesha kuwa, uchumi wa nchi zinazoendelea, isipokuwa China, unakadiriwa kushuka kwa asilimia 5.3 mwaka huu na kufufuka kwa asilimia 5 mwaka 2021, uchumi wa Marekani ukitarajiwa kushuka kwa asilimia 4.3 mwaka huu, huku uchumi wa China ukikadiriwa kukua kwa asilimia 1.9, ikiwa ni nchi pekee yenye uchumi mkubwa duniani inayoshuhudia ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako