• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaahidi kuongeza ufuatiliaji ili kukwepa mlipuko mpya wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-14 09:01:49

    Waziri Msaidizi wa Afya nchini Kenya Rashid Aman amesema, nchi hiyo itaongeza usimamizi na utekelezaji wa miongozo ya afya ya jamii ili kukwepa mlipuko mpya wa maambukizi ya virusi vya Corona wakati taasisi za elimu zikifunguliwa nchini humo.

    Bw. Aman amesema, ongezeko la hivi karibuni la maambukizi ya virusi hivyo na vifo limeleta wasiwasi mkubwa, hivyo kuonyesha haja ya kuimarisha zaidi hatua za udhibiti ili kukwepa hatari ya wimbi la pili la mlipuko.

    Amesema kulegezwa kwa hatua zilizolenga kudhibiti maambukizi ya virusi ikiwemo kufunguliwa tena kwa baa na shughuli nyingine za burudani huenda ndio chanzo cha maambukizi mapya. Ameongeza kuwa, serikali inaweza kurejesha hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi va Corona kama kufunga baa na kusitisha masomo ya darasani kama ikihakikisha kuna hatari ya kutokea wimbi la pili la mlipuko.

    Mpaka kufikia jana jumanne, kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya zilifikia 41,937, huku watu 787 wakifariki kutokana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako