• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya upinzani zaahidi kwa mara nyingine kusitisha mapambanao kwenye mazungumzo ya Roma

    (GMT+08:00) 2020-10-14 09:29:32

    Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya upinzani zimeahidi kwa mara nyingine kufuata Makubaliano ya Kusitisha Uhasama (COHA) katika mazungumzo ya amani yaliyomalizika hivi karibuni huko Rome.

    Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Sudan Kusini Bw. Barnaba Marial Benjamin amesema, wamekubaliana na makundi ya upinzani yaliyoongozwa na Muungano wa Harakati za Upinzani (SSOMA) kuhusu kufuata makubaliano ya kusitisha mapambano yaliyosainiwa mwezi Januari kabla ya kuanza kwa raundi ijayo ya mazungumzo kuhusu chanzo cha mogogoro nchini Sudan Kusini.

    Ameongeza kuwa, pande hizo mbili zitafanya tena mazungumzo tarehe 30 mwezi Novemba, ili kuendelea na majadiliano kuhusu masuala ya kisiasa ambayo ndio chanzo cha mgogoro nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako