• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 12 wa Mali wauawa kwenye mashambulizi katikati ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2020-10-14 09:30:00

    Jeshi la Mali jana limethibitisha kuwa, askari 12 wa nchi hiyo wameuawa kwenye mashambulizi yaliyofanywa na "makundi ya kigaidi" kati ya Jumatatu usiku na Jumanne asubuhi.

    Jeshi hilo limelengwa kwenye mashambulizi kadhaa tangu tarehe 18 mwezi Agosti lilipofanya mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa rais Boubacar Keita madarakani.

    Kabla ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Mali ipate uhuru, kiongozi wa Kamati ya Kitaifa ya Ukombozi wa Watu ambaye pia ni makamu wa rais wa mpito Assimi Goita, ameahidi kuwa jeshi la Mali litashinda vita dhidi ya makundi ya kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako