• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka nchi za Maziwa Makuu zihimize amani na maendeleo

    (GMT+08:00) 2020-10-14 10:25:21

    China imezitaka nchi za Maziwa Makuu barani Afrika zitumie fursa adimu ya kuhimiza amani na maendeleo katika eneo hilo.

    Hayo yamesemwa na naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing. Amesema hali katika eneo hilo imetulia na kuboreka katika miaka ya hivi karibuni, na kutoa fursa ya kuhimiza amani na maendeleo kwa nchi za eneo hilo.

    Ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, hali ya eneo hilo katika miezi sita iliyopita imekuwa nzuri, kwani uchaguzi mkuu nchini Burundi ulifanyika kwa amani, mageuzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yanaendelea kwa utulivu, uhusiano kati ya nchi za eneo hilo unaboreshwa hatua kwa hatua, na nchi za kanda hiyo ziko tayari kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani.

    Balozi Dai amesema ikiwa rafiki mkubwa na mwenzi mzuri wa nchi za Maziwa Makuu, China siku zote inaziunga mkono nchi hizo kusukuma mbele mchakato wa amani, na kushiriki katika shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, pamoja na kuzisaidia kujenga uwezo kadiri iwezavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako