• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China asisitiza kuhimiza mageuzi na ufunguaji mlango kwa kiwango cha juu

    (GMT+08:00) 2020-10-14 16:51:09
    Mkutano wa maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa eneo maalumu la kiuchumi la Shenzhen umefanyika leo mjini Shenzhen, na rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kuhutubia mkutano huo.
    Mwezi Disemba mwaka 1978, mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Awamu ya 11 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulitoa uamuzi wa kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Mwezi Agosti mwaka 1980, China ilianzisha maeneo maalumu ya kiuchumi katika miji ya Shenzhen, Zhuhai, Shantou na Xiamen, na mwezi Aprili mwaka 1988, ilianzisha eneo maalumu la kiuchumi mkoani Hainan. Maeneo hayo maalumu ya kiuchumi yamekuwa madirisha muhimu ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango na ujenzi wa mambo ya kisasa nchini China.
    Rais Xi akihutubia mkutano huo amejulisha uzoefu uliopatikana kwenye maeneo maalumu ya kiuchumi kuhusu mageuzi na ufunguaji mlango, na kupata maendeleo ya kivumbuzi katika miaka 40 iliyopita akisema:
    "Ni lazima kushikilia ufunguaji mlango kwa pande zote, kuchukua uvumbuzi uwe msukomo wa kwanza, kushikilia wazo la kujiendeleza kwa kutoa kipaumbele kwa wananchi, na kutekeleza wazo la "mazingira mazuri ni utajiri", tena ni lazima kutekeleza mwongozo wa kimsingi wa 'Nchi moja, Mifumo miwili'."
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako