• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia kutoa dola za kimarekani bilioni 12 kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya chanjo na matibabu ya Corona

    (GMT+08:00) 2020-10-14 17:52:43

    Benki ya Dunia jana ilitangaza kuwa bodi ya utendaji ya benki hiyo iliidhinisha kutoa dola za kimarekani bilioni 12 kwa nchi zinazoendelea ili kuzisaidia kununua na kusambaza chanjo za Corona, kufanya upimaji na matibabu ya virusi vya Corona.

    Mkuu wa benki hiyo Bw. David Malpass katika taarifa iliyotolewa na benki hiyo alisema kuwa, benki ya dunia inachukua hatua ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata chanjo ya Corona kwa usawa na haki.

    Shirika la Mfuko wa Fedha la Kimataifa IMF siku hiyo lilitoa ripoti ya makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia ikionesha kuwa, maendeleo ya upimaji na matibabu ya virusi vya Corona na uchunguzi wa chanjo na sera nyingine yataweza kuboresha mustakabali wa maendeleo ya uchumi. Lakini janga la COVID-19 huenda litarudia tena, kama mustakabali ya matibabu na uchunguzi wa chanjo ukizidi kuwa mbaya, shughuli za uchumi za dunia zitaathiriwa vibaya, na huenda zitaongeza msukosuko wa soko la fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako