• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu maskini zaidi ya milioni 9.6 nchini China wahamia nyumba mpya katika miaka 5 iliyopita

    (GMT+08:00) 2020-10-14 18:37:44

    Mkurugenzi wa Idara ya ustawi wa kikanda katika Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Tong Zhangshun leo amesema, kutokana na juhudi za miaka 5 iliyopita, watu masikini zaidi ya milioni 9.6 kote nchini China wamehamia nyumba mpya, na kazi ya ujenzi wa kuwasaidia watu maskini kupitia uhamisho katika "mpango wa 13 wa miaka mitano" imekamilika.

    Bw. Tong amesema, katika miaka mitano iliyopita, China imejenga maeneo elfu 35 na nyumba zaidi ya milioni 2.66 za kuwaweka watu maskini, na watu masikini zaidi ya milioni 9.6 wamehamia nyumba mpya. Bw. Tong amesema hivi sasa mpango wa kuwasaidia watu maskini kwa kupitia uhamisho umeingia kipindi kipya, sera za kuwasaidia watu maskini kwa maendeleo ya viwanda, ajira, usimamizi wa mitaa na usajili wa nyumba zimetolewa na kupata ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako