• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yaanza majaribio ya chanjo ya MMR dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-14 18:42:57

    Wanasayansi wa vyuo vikuu vya Cape Town na Witwatersrand nchini Afrika Kusini jana walianza majaribio ya kikliniki ili kuangalia kama chanjo za utotoni za surua, matumbwitumbwi na rubella MMR zinaweza kulinda watumishi wa afya walio mstari wa mbele kupambana na COVID-19 au kupunguza makali ya ugonjwa kwa wale wanaoambukizwa.

    Profesa Bruce Biccard wa Chuo kikuu cha Cape Town amesema kama watagundua kwamba chanjo za MMR zinaweza kusaidia kuleta mwitikio kwenye kinga ya mwili kwa maambukizi ya SARS-CoV-2, basi watakuwa na kitu cha kutumia kwa sasa wakati wakisubiri chanjo husika na tiba za kuzuia kuendelezwa.

    Kuna ushahidi mkubwa unaoonesha kuwa chanjo za MMR zinaweza kusaidia hata na magonjwa mengine. Zina uwezo wa kuongeza kinga ya mwili na kuzuia maambukizi ya virusi vya SARS-CoV-2 vinavyosababisha COVID-19 kwa muda fulani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako