Uganda imeanza kutoa huduma ya kingamwili kwa watoto na watu wazima zaidi ya milioni 38.4 ambao walikosa huduma za chanjo ya lazima kutokana na zuio la COVID-19.
Msemaji wa Wizara ya Elimu Emmanuel Ainebyoona amesema wizara yake inaendesha kampeni ya chanjo ya Oktoba, inayoitwa Siku za Kukamilisha Afya ya Mtoto, ili kupunguza magonjwa yanayozuilika, vifo na ulemavu yanayotokana na kuharisha, nimonia, surua, tetenasi, kifua kikuu na saratani ya kizazi, miongoni mwa mengine.
Bw. Ainebyoona amesema jumla ya watoto wa kike milioni 1.2 wenye umri kati ya miaka 10 na 11 wanapatiwa kinga ya saratani ya kizazi, watoto milioni 17.3 wenye umri chini ya miaka 15 wanapewa tiba ya kuondoa minyoo, na watoto milioni 7.5 wenye umri chini ya miaka mitano wanapaswa kupokea dawa za Vitamin A ili kuwalinda na upofu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |