• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuchaguliwa tena China kwaonyesha jumuiya ya kimataifa inatambua maendeleo ya haki za binadamu nchini China

    (GMT+08:00) 2020-10-14 20:10:57

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China imechaguliwa kwa mara ya tano kuwa nchi mwanachama wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, na hiyo inaonyesha kuwa jumuiya ya kimataifa imekubali maendeleo ya mambo ya haki za binadamu nchini China na ushiriki wa China katika usimamizi wa haki za binadamu duniani.

    Bw. Zhao Lijian amesema, serikali ya China inatilia maanani sana kuhimiza na kulinda haki za binadamu, kushikilia wazo la kuweka kipaumbele maslahi ya wananchi, na kufanikiwa kupata njia ya kuendeleza haki za binadamu yenye umaalumu wa Kichina. China inatekeleza kwa makini wajibu wake wa kimataifa wa haki za binadamu, na kufanya mazungumzo na ushirikiano na nchi mbalimbali kuhusu haki za binadamu.

    Amesema China itatumia fursa hii ya kuchaguliwa kuwa nchi mwanachama wa baraza hilo, kuendelea kushiriki kwenye kazi za mfumo wa haki za binadamu za Umoja wa Mataifa, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya maendeleo ya mambo ya haki za binadamu ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako