Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohammed ametoa wito wa juhudi zote kufanywa ili kutatua msukosuko wa tabianchi ambao ameutaja kuwa umeingia kwenye kipindi kipya cha machafuko.
Akiongea kwenye mkutano wa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) uliofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu uwekezaji binafsi, Bi. Amina Mohammed amehimiza juhudi zote zifanywe katika kutimiza lengo la utoaji sifuri wa gesi ya ukaa ifikapo mwaka 2050 ili kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijoto 1.5.
Ofisa huyo amepongeza tangazo la China lililotolewa kwenye Mjadala Mkuu wa Kikao cha 75 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa nchi hiyo inalenga kutimiza uwiano kati ya uzalishaji na unyonyaji wa gesi ya ukaa (Carbon-neutral) kabla ya mwaka 2060 na kufikia kilele cha utoaji wa gesi hiyo kabla ya mwaka 2030.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |