Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametangaza kuwa amri ya kutotoka nje kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12 asubuhi, itaanza kutekelezwa kwenye eneo kuu la Paris na miji mingine minane nchini humo kuanzia Ijumaa kwa muda wa wiki nne, ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.
Hatua hiyo imekuja baada ya Ufaransa kushuhudia wimbi la pili la mlipuko wa virusi vya Corona ambapo wastani wa maambukizi mapya elfu 20 yanaripotiwa kila siku.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |