• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yaomboleza wahanga wa mashambulizi ya Oktoba 2017 huku ikitoa wito wa umoja na uvumilivu

    (GMT+08:00) 2020-10-15 09:17:01

    Jamii ya kimataifa jana imeungana na Somalia kuomboleza vifo vya watu 587 waliouawa na wengine 316 kujeruhiwa katika mashambulizi mabaya zaidi ya mabomu yaliyotokea Oktoba 14, 2017 mjini Mogadishu.

    Maofisa wa serikali ya Somalia, wabunge na maofisa wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wamewataka wananchi wa Somalia kuendelea kuvumiliana na kujenga umoja ili kusaidia kuwa na amani ya kudumu nchini humo.

    Waziri wa Fedha wa Somalia Abdirahman Beileh amesema, licha ya kitendo hicho cha kigaidi, Mogadishu na Somalia yote kwa ujumla imeendelea na njia ya kutafuta amani na ustawi. Akitoa heshima zake kwa wahanga wa mashambulizi hayo, Bw. Beileh amesema Somalia ina nguvu zaidi na inajijenga upya kwa pamoja na kwa ubora zaidi.

    Naye mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia James Swan amesema, familia ya Umoja huo iko pamoja na Somalia katika kujenga mkakati wa baadaye wa amani, utawala bora na ustawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako