• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wanawake barani Afrika wataka hatua zichukuliwe kuondoa ukosefu wa usawa katika sekta ya afya wakati wa janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-15 09:17:20

    Viongozi wanawake kutoka Afrika kusini mwa Sahara wamezitaka serikali za kanda hiyo kukabiliana na ukosefu wa usawa katika huduma za afya ambazo zimekuwa mbaya zaidi wakati wa janga la virusi vya Corona.

    Wakizungumza katika mkutano wa afya uliofanyika kwa njia ya video, viongozi hao wamesema sera imara na sheria zinatakiwa ili kukabiliana na janga hilo linaloathiri wanawake na wasichana katika bara la Afrika.

    Mke wa rais wa Namibia Bi. Monica Geingos amesema, virusi vya Corona vimeweka bayana ukosefu wa usawa wa kijinsia katika upatikanaji wa huduma za afya barani Afrika, kwa kuvuruga huduma za wamama wanaojifungua hospitalini na huduma za uzazi wa mpango.

    Naye Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa katika Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika Bi. Matshidiso Moeti amesema, kukabiliana na ukosefu wa usawa wa jinsia ni ufunguo muhimu katika ufufukaji wa kiuchumi wa bara hilo baada ya janga la virusi vya Corona. Amesema nafasi muhimu ya wanawake katika kutimiza upatikanaji wa huduma ya afya kwa wote barani Afrika imethibitika tena wakati wa janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako