• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ethiopia atoa wito wa kuwa na mfumo wa kisasa wa takwimu katika bara la Afrika

    (GMT+08:00) 2020-10-15 09:17:39

    Rais Sahle-Work Zewde wa Ethiopia amelitaka bara la Afrika kuweka mifumo ya kisasa ya takwimu itakayowezesha kutoa maamuzi sahihi na kutunga sera makini katika wakati huu ambao janga la virusi vya Corona linaendelea kuikabili Afrika.

    Rais Zewde amesema hayo katika mkutano wa Tume ya Takwimu ya Afrika (StatCom) uliofanyika kwa njia ya video. Amelitaka bara la Afrika kufanya mageuzi ya dharura na kuifanya mifumo yake ya takwimu kuwa ya kisasa, hususan katika wakati huu wa janga la virusi vya Corona.

    Pia amesema, serikali za nchi za Afrika zinahitaji kuunga mkono zaidi na kutenga bajeti kwa ajili ya kukarabati ofisi za takwimu kuwa za kisasa kwa ajili ya mipango na maamuzi yanayotokana na mambo halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako