• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yasema COVID-19 imeleta athari kubwa kwa uchumi jamii ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-10-15 09:17:58

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema, janga linaloendelea la virusi vya Corona limesababisha athari mbaya kwa uchumi na jamii ya Afrika.

    Akizungumza katika Mkutano wa 37 wa Kawaida wa Baraza Kuu la Umoja wa Afrika uliofanyika kwa njia ya video, Bw. Mahamat amesisitiza kuwa janga la virusi vya Corona limedhoofisha zaidi mifumo ya afya barabi Afrika ambayo tayari ilikuwa dhaifu.

    Hata hivyo, Bw. Mahamat amesema nchi za Afrika zimepiga hatua kubwa katika kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo tangu vitokee barani Afrika mwezi Machi mwaka huu.

    Mpaka kufikia jana mchana, takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika zilionyesha kuwa, kesi za virusi vya Corona barani humo zimefikia 1,592,549.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako