• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Guinea ya Ikweta watumiana salamu za pongezi kwa kutimiza miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2020-10-15 09:24:25

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema wametumiana salamu za pongezi kwa kutimiza miaka 50 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Kwenye salamu zake, rais Xi amesema, katika miaka 50 iliyopita, bila kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa, China na Guinea ya Ikweta zimetendeana kwa udhati na urafiki, na kuungana mkono kithabiti katika maslahi makuu na masuala yanayofuatiliwa na nchi hizo, na wananchi wa nchi hizo wamenufaika na ushirikiano kati ya pande hizo. Rais Xi amesema, tangu kutokea kwa mlipuko wa COVID-19, China imeshikamana na kusaidiana na nchi za Afrika ikiwemo Guinea ya Ikweta ili kupambana na janga hilo kwa pamoja. Ameongeza kuwa anapenda kushirikiana na rais Obiang kuimarisha zaidi uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Obiang amesema, nchi yake inaridhika na maendeleo ya uhusiano kati yake na China, na kupenda kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati yake na China.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na mwenzake wa Guinea ya Ikweta Simeon Oyono Esono Angue pia wametumiana salamu za pongezi kwa kutimiza miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako