• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuweka kipaumbele katika uhifadhi wa mazingira wakati wa kuendeleza viwanda

    (GMT+08:00) 2020-10-15 09:40:02

    Katibu mkuu wa wizara ya viwanda ya Kenya Bw. Francis Owino jana amesema, Kenya itaweka kipaumbele katika uhifadhi wa mazingira kwenye mchakato wa kuendeleza viwanda, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutimiza maendeleo endelevu.

    Bw. Owino amesema mabadiliko ya tabianchi ni moja ya matishio makubwa zaidi yanayoikabili Kenya, ambayo yanaweza kufuta mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyopatikana nchini humo.

    Katika maadhimisho ya Siku ya Vigezo Duniani, Bw. Owino amesema wakati Kenya inapohimiza maendeleo ya viwanda, itafuata vigezo vya mazingira ili kulinda ubora wa hewa, maji na udongo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako