• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha Joachim Low asema panga pangua watafika nusu fainali ya michuano ya Euro

    (GMT+08:00) 2020-10-15 16:30:59

    Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amesema kikosi chake lazima kifike hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya Euro mwakani. Timu ya taifa ya Ujerumani ilitoka sare ya bao 3-3 dhidi ya timu ya taifa ya Uswisi kwenye mchezo wa michuano ya UEFA Nations league, Sare hiyo ni ya 4 kwa mabingwa hao wa Dunia mara 4 katika michezo 5 ya mwisho waliyocheza na wameshinda mchezo mmoja tu.

    Licha ya kikosi hicho kuwa na mapungufu katika mchezo huo hususani eneo la ulinzi, baada ya mchezo huo kumalizika kocha Joachim Low alisema walifanya makosa kadhaa kwenye safu ya ulinzi, lakini wanahitaji kurekebisha makosa hayo. Sasa Ujerumani wanashika nafasi ya pili kwenye kundi namba 4 la UEFA Nation League wakiwa na alama 6, tofauti ya alama 1 na vinara timu ya taifa ya Hispania wenye alama 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako