• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Juan Mata akata ofa ya mkwanja mnene kuhamia Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2020-10-15 16:31:24

    Juan Mata anaripotiwa kukataa ofa kubwa ya pauni milioni 18 kuhamia katika klabu moja ambayo haikutajwa ya Saudi Arabia. Mata kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akitupwa mkekani na hajashirikishwa katika mechi ya Man United. Hata hivyo, alishirikishwa katika mechi mbili ya United ikiwemo Kombe la Carabao ambapo alichangia pakubwa katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Brighton na kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo. Na katika kujaribu kumnasua kwenye masaibu yanayomkumba ugani Old Trafford, MailSport inaripoti kuwa Muhispania huyo alikabidhiwa ofa ya pauni milioni 11.5 kuhamia katika timu ya Saudia. Kulingana na gazeti hilo likinukuu shirika la Uhispania la AS, ofa hiyo iliongezwa hadi pauni milioni 18 lakini Mata alikataa kuhama. Inaaminika kuwa mkali huyo wa zamani wa Chelsea hana hamu ya kuhama na ana matumaini kuwa huenda United itashinda taji msimu huu. Hii ni licha ya Manchester United kuendelea kujikokota tangu kuanza kwa kampeni mpya na kusajili ushindi mmoja pekee dhidi ya The Seagulls.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako