• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya 128 ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China yafunguliwa

    (GMT+08:00) 2020-10-15 16:38:26

    Maonesho ya 128 ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China yamefunguliwa leo kwenye mtandao. Maonesho hayo yatakayoendelea kwa siku 10, yamevutia viwanda elfu 26 kutoka nchini na nje ya nchi kushiriki.

    Maonesho hayo yameweka maeneo 50 ya maonesho ambayo yanagawanywa kwa aina 16, idadi ya vibanda imefikia elfu 60 ambavyo vitashirikisha viwanda karibu elfu 26. Bidhaa zote zitaoneshwa kuanzia leo hadi tarehe 24 kwenye mtandao wa Internet.

    Viwanda na mashirika viwe kutoka nchini au nje ya nchi , wateja wapya au waliowahi kushiriki kwenye maonesho hayo yaliyopita, wote wana matumaini makubwa juu ya maonesho hayo. Mteja kutoka Jamaica Bw. Charles Simmons amesema, anashiriki kwenye maonesho hayo kila mwaka, akiona kuwa hii ni fursa nzuri ya kupanua mawasiliano ya kibiashara na China. Anasema:"Niligundua maonesho haya karibu miaka 15 iliyopita, na kuanzia hapo maisha yangu yakapata mabadiliko makubwa. Nimegusa teknolojia mpya, mwelekeo mpya, na biashara yangu imenufaika sana. Maonesho hayo yamefungua soko jipya, hali ambayo imeniwezesha kuwasiiana na makampuni ya utengenezaji. Natarajia kukutana tena na makampuni mapya na yale yaliyowahi kutoa bidhaa kila mwaka kwenye maonesho hayo."

    Ikiwa alama ya mwelekeo wa biashara nje ya China, maonesho hayo ya mwaka huu yataendelea kuonesha umuhimu wake kama jukwaa la ufunguaji mlango kwa nje kwa pande zote, na kuvisaidia viwanda kupanua masoko ya kimataifa, kuhimiza mzunguko mzuri wa mnyororo wa utoaji wa bidhaa kwenye minyororo ya biashara ya nje, ili kuongeza imani ya pande zote.

    Msemaji wa maonesho hayo na naibu mkurugenzi wa Kituo cha biashara ya nje ya China Bw. Xu Bing ameeleza kuwa maonesho hayo ya mwaka huu yataboresha ufanisi wa maonesho ya bidhaa, na kufanya juhudi za kuleta uzoefu mpya kwa washiriki. Vilevile yatawavutia wafanyabiashara wenye kiwango cha juu kutoka nchi na sehemu nyingi zaidi kwa kutoa mialiko kupitia mtandao wa Internet, na kufanya matangazo makubwa. Anasema:"Tutafanya matangazo kupitia mtandao wa Internet juu ya masoko muhimu yakiwemo ya Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi zinazojiunga na pendekezo la 'Ukanda mmoja, Njia moja'."

    Pia ameeleza kuwa maonesho hayo yatatafuta njia ya kufanya mawasiliano kupitia mtandao wa Internet kati ya viwanda vinavyoshiriki kwenye maonesho na wanunuzi katika nchi za Ufaransa, Ukraine, Falme za Kiarabu na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako