• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Qingdao, China kukamilisha kampeni ya upimaji virusi vya Corona kwa watu milioni 11

    (GMT+08:00) 2020-10-15 18:20:12

    Baada ya maambukizi mapya ya COVID-19 kuibuka katika mji wa Qingdao uliopo mkoani Shandong, mji huo umeapa kukamilisha kampeni ya kupima virusi vya Corona kwa njia ya nucleic acid ambayo itajumuisha wakazi milioni 11 katika mji mzima ndani ya siku tano kuanzia Jumatatu.

    Hadi kufikia leo saa 2 asubuhi, zaidi ya watu milioni 9.94 wamechukuliwa sampuli huku zaidi ya sampuli milioni 7.64 kati ya zilizokusanywa zimepimwa.

    Ukiachilia mbali maambukizi ambayo tayari yalisharipotiwa, hakuna mgonjwa mpya aliyegundulika katika sampuli mpya. Virusi vya Corona ambavyo viliibuka hivi karibuni vimepelekea kuwa na wagonjwa wapya 13 wa COVID-19 hadi jana Jumatano. Wagonjwa wengi wapya wanahusishwa na Hospitali ya Kifua ya Qingdao, ambayo imekuwa ikitumika kuwatibu wagonjwa wa COVID-19 waliotoka nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako