• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya nje ya Uganda kwenda Kenya yapungua kutokana na ucheleweshaji mipakani

    (GMT+08:00) 2020-10-15 18:20:32

    Uingiaji wa bidhaa za Uganda nchini Kenya ulipungua mwezi Agosti kutokana na ucheleweshaji na na upungufu wa shughuli za kiuchumi kufuatia mlipuko wa janga la Covid-19.

    Kulingana na Shirika la Takwimu la Uganda,mauzo ya nje ya Uganda kwenda Kenya mwezi Agosti yalikuwa $46.9 million (Sh5.1 billion)ikiwa mauzo hayo yamepungua kidogo kutoka $48.3 million (Sh5.2 billion)katika kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Kwa upande mwengine,thamani ya mauzo ya Kenya kwenda Uganda iliongezeka hadi $88 milioni (Sh9.6 billion ) kutoka $53.9 million (Sh5.9 billion ) katika kipindi sawa na hicho mwaka jana ,licha ya kuwa ucheleweshaji unazidi kuathiri usafirishaji wa bidhaa.

    Bidhaa kuu ambazo Kenya huagiza kutoka Uganda ni pamoja na maziwa,tumbaku,miwa,nishati na mbao,miongoni mwa bidhaa nyingine.

    Bidhaa zinazoagizwa na Uganda kutoka Kenya ni mafuta ya nazi,chuma,bidhaa za petrol,chumvi,pamoja na bidhaa nyengine.

    Utendaji huo umejiri kutokana na michakato ya polepole ya upitishaji bidhaa katika mipaka ya nchi hizo mbili,kutokana na miongozo iliyowekwa ya kudhibiti usambaaji wa virusi vya korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako