• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Benki ya Dunia atoa mwito wa kuzidi kuunga mkono nchi maskini

    (GMT+08:00) 2020-10-15 18:20:32

    Mkuu wa Benki ya Dunia Bw. David Malpass jana alisema, maambukizi ya virusi vya Corona na hatua za zuio zilizochukuliwa na serikali za nchi mbalimbali zimesababisha hali ya kutokuwa na usawa, hasa zimeleta pigo kubwa zaidi kwa nchi zinazoendelea na watu maskini. Amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuendelea kuzidi kuunga mkono makundi ya kiuchumi yaliyoko nyuma kimaendeleo, na kutafuta utatuzi wa muda mrefu na endelevu kwa mgogoro wa madeni.

    Bw. Malpass amesema hayo kwenye Mkutano wa mawaziri wa mambo ya fedha na wakuu wa benki kuu wa nchi za G20 kwa njia ya video, akibainisha kuwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, uchumi wa makundi mengi ya kiuchumi yanayoendelea unadidimia. Hadi kufikia mwaka 2021, idadi ya watu maskini kabisa duniani huenda itaongezeka milioni 150.

    Mkutano huo umetoa taarifa ya pamoja na kukubali kuahirisha kwa miezi 6 zaidi nchi maskini kulipa madeni, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2021, ili kuziunga mkono kupambana na virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako