• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chuo cha Uhasibu Arusha ,IAA chaanza kutoa mafunzo kwa mawakala wa benki

    (GMT+08:00) 2020-10-15 18:20:50

    Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), kimeanza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya mawakala wa benki na wanaoendesha huduma za fedha kwa njia ya simu kutokana na sekta hizo kukua kwa kasi nchini.

    Aidha, chuo hicho kinatarajia kufungua tawi lake jijini Dodoma mwishoni mwa mwaka huu kwa ngazi ya shahada ya uzamivu na mafunzo hayo ya muda wa wiki sita.

    Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Arusha, Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka, alisema mafunzo hayo yanalenga kuchochea masuala ya kiuchumi ili kuwapo na uchumi shirikishi wenye weledi na ujuzi.

    Alibainisha kuwa katika Mpango Mkuu wa Maendeleo Sekta ya Fedha nchini wa miaka 10, taasisi za elimu ya juu nchini na taasisi za utafiti zimeagizwa kutumia fursa zilizo kwenye mpango huo, ili kujipanga katika kuboresha maeneo ya kitaalamu na kiutafiti ili sekta iendelee kukua na kuhimili ushindani na mabadiliko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako