Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha Duniani IMF Bibi Kristalina Georgieva jana katika mkutano wa mwaka wa shirika hilo alisema kuwa, hivi sasa uchumi wa dunia unafufuka baada ya kukumbwa na msukosuko, hivyo nchi mbalimbali zinapaswa kuimarisha ushirikiano na kukabiliana na msukosuko huo kwa pamoja.
Bibi Georgieva alisema kuwa, mapambano dhidi ya janga la COVID-19 yameendelea kwa miezi 9 ambalo limesababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 1 pia likiyumbisha uchumi wa dunia. Shirika hilo lilikadiria kuwa, uchumi wa dunia wa mwaka 2020 utapungua kwa asilimia 4.4.
Bibi Georgieva alisisitiza kuwa ushirikiano wa kimataifa ni muhimu sana katika kukabiliana na msukosuko huo, hasa katika sekta ya utafiti na usambazaji wa chanjo ya COVID-19.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |