• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watoa dola milioni 10 kuisaidia Sudan Kusini kukabiliana na mafurikio

    (GMT+08:00) 2020-10-16 08:44:45

    Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa dola za kimarekani milioni 10 kuunga mkono msaada wa kuokoa maisha kwa watu laki 3.6 walioathiriwa na mafurikio nchini Sudan Kusini.

    Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Alain Noudehou amesema fedha zilizotolewa na mfuko huo zitawezesha familia zilizoathirika kupata msaada wa dharura, ikiwemo chakula, makazi ya muda na maji safi.

    Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya dola za kimarekani milioni 80 zinahitajika kukabiliana na mafuriko nchini Sudan Kusini kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako