Jukwaa la biashara ya mtandaoni la Afrika (Jumia) linatafuta kupanua ushirikiano na wazalishaji wa China, ili kuongeza mapato yao.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Kenya Bw. Sam Chappatte amesema, China ni mzalishaji wa bidhaa mwenye ufanisi na kampuni za China zinatoa bidhaa zenye ubora na bei nafuu kwa wateja wa Afrika. Ameongeza kuwa kampuni yake ni mwenzi mzuri kwa wazalishaji wa China kwa kuwa inawawezesha kuwafikia moja kwa moja wateja wa Afrika, na kwamba imekuwa moja ya majukwaa maarufu zaidi ya biashara ya mtandaoni barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |