Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Ulaya Dkt. Hans Kluge amesema bara la Ulaya linatakiwa kuongeza hatua sahihi ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.
Akizungumza na wanahabari kupitia mtandao, Dkt. Kluge amesema virusi hivyo kwa sasa ni chanzo cha tano cha vifo, na kuthibitisha kuwa kesi za maambukizi hayo barani Ulaya imepita milioni saba, huku maambukizi mapya laki 7 yairipotiwa wiki iliyopita.
Ameeleza wasiwasi wake kuwa, kulegezwa kwa hatua binafsi za kujikinga ama sera kunaweza kusababisha kuongezeka kwa idadi ya vifo itakapofika Januari mwakani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |