• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 12 wafariki kutokana na mafuriko ya ghafla nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-10-16 09:03:02

    Watu 12 wamefariki katika mafuriko ya ghafla yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, Tanzania.

    Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa imesema, watu hao walifariki baada ya kusombwa na mafuriko, wakiwemo watoto wawili wa familia moja.

    Taarifa hiyo hiyo pia imesema, watu watano wa familia moja wamefariki jumanne baada ya nyumba yao kuungua moto katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam, na kusema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.

    Wakati huohuo, Wizara ya Afya nchini Tanzania imetoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko, ikiwemo homa ya dengu na kipindupindu kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini humo.

    Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amewataka watu kuchukua tahadhari za kiafya kama kunywa maji yaliyochemshwa na kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka na sabuni kuepuka na magonjwa hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako