• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi za COVID-19 barani Afrika zapita milioni 1.6

    (GMT+08:00) 2020-10-16 09:03:23

    Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) zimeonyesha kuwa, kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika mpaka kufikia jana alhamis ni 1,603,982.

    Taarifa iliyotolewa na Kituo hicho imesema, idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi hivyo ni 39,122, na watu 1,325,204 wamepona.

    Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maambukizi kwa mara ya kwanza katika miezi saba iliyopita, Mkurugenzi wa Kituo hicho John Nkengasong ameonya dhidi ya kulegea kwa mapambano dhidi ya virusi hivyo.

    Nkengasong amezitaka nchi za Afrika kudumisha mapambano dhidi ya janga hilo, licha ya jamii kuchoshwa na hasara za kiuchumi zinazosababishwa na hatua zilizowekwa na serikali za nchi za Afrika katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako