• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Somalia lawauwa wapiganaji 61 wa al-Shabab

    (GMT+08:00) 2020-10-16 09:10:29

    Jeshi la Somalia limewaua wapiganaji 61 wa kundi la al-Shabab katika mapambano yaliyotokea karibu na mji wa Afgoye, umbali wa kilomita 30 magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

    Msemaji wa jeshi hilo Dhame Sadik Adan, amesema wanajeshi 18 waliuawa baada ya wapiganaji wa al-Shabab kuwashambulia kwa ghafla askari wa Jeshi la Somalia (SNA) waliokuwa wakifanya doria katika eneo karibu na mji wa Afgoye Jumatano alasiri.

    Tukio hilo ni moja ya mashambulizi mabaya zaidi ya mwaka huu yaliyofanywa na kundi la al-Shabab, ambalo limeongeza mashambulizi dhidi ya serikali na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia katika maeneo ya kusini na katikati mwa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako