• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanane wauawa katika maandamano kwenye jimbo la Kassala nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2020-10-16 09:27:21

    Serikali ya Sudan jana ilitangaza kuwa watu wanane waliuawa katika maandamano yaliyotokea kwenye jimbo la Kassala, mashariki mwa nchi hiyo.

    Waziri wa habari wa Sudan ambaye pia ni msemaji wa serikali Bw. Faisal Mohamed Saleh aliwaambia waandishi wa habari kuwa, askari mmoja ni miongoni mwa watu waliouawa katika mapigano hayo kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama.

    Alisema kuwa serikali ya Sudan iliamua kutangaza hali ya hatari ya siku tatu huko Kassala.

    Maandamano hayo yamefanyika kupinga uamuzi wa hivi karibuni wa Waziri Mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok kumfukuza kazi gavana wa serikali ya jimbo hilo Bw. Saleh Ammar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako