• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Usalama la UM lapongeza mipango ya kisiasa ya mpito nchini Mali

  (GMT+08:00) 2020-10-16 09:37:35

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limetoa taarifa likipongeza mipango ya kisiasa ya mpito nchini Mali, na kusisitiza haja ya kutekeleza mipango hiyo kwa pande zote.

  Kwenye taarifa hiyo, Baraza hilo limepongeza uteuzi wa rais wa mpito, makamu wake, waziri mkuu na serikali nchini Mali, na pia kutoa mkataba wa mpito. Pia Baraza hilo limepongeza kuachiliwa kwa maafisa wote walioshikiliwa, kulingana na ombi la Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), na kutoa wito wa kuunda haraka Baraza la Mpito la Kitaifa.

  Baraza la Usalama limeisifu ECOWAS kwa ahadi na juhudi za usuluhishi nchini Mali, ikizingatia taarifa iliyotolewa na Jumuiya hiyo tarehe 5 mwezi huu kuhusu mipango ya mpito na uondoaji wa vikwazo vyake vilivyowekwa hapo awali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako