Jeshi la Pakistan jana limesema, watu 20 wameuawa katika mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotokea nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema, jana alhamis, msafara wa Kampuni ya mafuta na gesi ya Pakistan ulishambuliwa na wapiganaji wengi wa kigaidi kwenye barabara ya pwani katika Mji wa Olmara, ambapo askari 7 wa ulinzi wa mpaka na walinzi 7 waliuawa kwenye mapambano hayo.
Taarifa nyingine iliyotolewa na jeshi la Pakistan imesema, magaidi walishambulia msafara wa jeshi la Pakistan kwa kutumia mabomu ya kienyeji (IEDs) karibu na mji wa Razmog, na kuwaua wanajeshi 6.
Kundi la Taliban nchini Afghanistan limetangaza kuwajibika na shambulizi hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |