• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara ya mipaka Afrika mashariki yadorora kutokana na ukosefu wa vifaa vya kupima Covid 19

    (GMT+08:00) 2020-10-16 16:44:08

    Upungufu wa vifaa vya kupima virusi vya Corona katika mipaka ya Busia na Malaba umesababaisha msongamano mkubwa wa malori katika maeneo hayo. Msongamano huo ambao unadaiwa kuwa wa kilomita 30 umeathiri biashara kwa kiwango kikubwa kati ya nchi za Afrika mashariki. Kundi la wafanyabiashara katika nchi zote za Afrika mashariki limezitaka nchi hizo kuongeza vifaa vya kupima virusi vya Corona ili kuzuia hali hiyo isiendelee. Hivi sasa kuna msongamano mkubwa wa malori yanayoelekea katika mpaka wa Busia kuanzia mji wa Mundika uliopo umbali wa kilomita 15 huku msongamano katika mpaka wa Malaba ukiza zaidi ya kilomita 30. Kundi hilo la wafanya biashara wa Afrika mashariki pamoja na wizara ya Afrika mashariki nchini Kenya imezitaka nchi wanachama kuzuia msongamano unaotokana na kucheleweshwa kwa utoaji vyeti vya kuonyesha kudhibitisha hali yako ya corona. Ucheleweshwaji huo umepelekea malori 2400 yanayoelekea Uganda kukwama hali ambayo imeathiri pakubwa biashara katika maeneo ya mipakani. Kundi la wafanya biashara wa Afrika mashariki limesema madereva wengi wa Uganda husafiri bila vyeti vya kuonyesha hali yao ya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako