• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpango wa kufufua uchumi wa rais wa Afrika Kusini wakaribishwa

  (GMT+08:00) 2020-10-16 16:44:42

  Wachumi wa Afrika Kusini na sekta ya kazi jana walikaribisha mpango mpya wa kufufua uchumi uliotangazwa na rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, wakisema unaweza kuharakisha ukuaji wa uchumi wa nchi kama ukitekelezwa ipasavyo.

  Akizindua mpango huo bungeni jana mapema wakati ambapo ukuaji wa uchumi wa nchi unakadiriwa kupungua kwa asilimia 8 mwaka 2020 kutokana na athari za COVID-19, Ramaphosa amesema Afrika Kusini itatumia zaidi ya randi bilioni 100 sawa na dola bilioni 6 za kimarekani katika miaka mitatu ijayo kutoa nafasi za ajira kupitia ajira za umma na kijamii wakati ambapo soko la ajira linafufuka.

  Mkuu wa Kituo cha Uchumi na Sayansi ya Biashara cha Chuo kikuu cha Witatersrand Jannie Rossouw amesema ni mpango kamili wa kina unaokabiliana na masuala mengi muhimu yanayoikabili nchi. Wakati huohuo Baraza la Vyama vya Wafanyakazi la Afrika Kusini COSATU, limesema linakaribisha mpango huo huku likionya kuhusu ufisadi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako