• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi wa WFP nchini China: Inapaswa kujulisha uzoefu wa China katika kupunguza umaskini kwa nchi nyingine duniani

    (GMT+08:00) 2020-10-16 16:48:12

    Leo tarehe 16 ni Siku ya Chakula Duniani, kauli mbiu ya mwaka huu ni "kupata maendeleo na ustawi kwa pamoja, kujenga mustakabali kwa vitendo halisi". Likiwa shirika kubwa zaidi la utoaji wa misaada ya kibinadamu kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP linatoa msaada kwa watu milioni 90 kwenye nchi zipatao 80 duniani. Mwakilishi wa shirika hilo nchini China Bw. Qu Sixi ameeleza kuwa, China imetoa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea katika kupunguza umaskini.

    Kuanzia mwaka 1979, tangu shirika la WFP lilipoingia nchini China, limeshuhudia China ikiondokana na umaskini na kupata ukuaji wa uchumi. Bw. Qu anaona kuwa, China imetoa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea kuondoa umaskini. Anasema:"Bila shaka, China ni nchi inayotoa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea duniani kupunguza umaskini. Tangu sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ilipoanza kutekelezwa hadi sasa, China imewasaidia watu zaidi ya milioni 800 wenye matatizo ya kiuchumi kuondoa umaskini, hali ambayo imechangia mambo ya kuondoa umaskini duniani, na uzoefu mkubwa uliopatikana na China unaweza kusomwa na nchi nyingine zinazoendelea. Mafanikio kama hayo pia yametia moyo kwa nchi nyingine zinazoendelea."

    Shirika la WFP liliwahi kutekeleza miradi zaidi ya 70 ya kupunguza umaskini na ukarabati baada ya maafa nchini China. Kutokana na ukuaji wa kasi wa uchumi na mchakato wa kupunguza umaskini nchini China, miradi hiyo imekamilishwa mwaka 2005, na China imebadilika kutoka nchi inayopewa msaada wa chakula kuwa nchi kubwa inayotoa msaada kwenye operesheni ya WFP duniani. Bw. Qu anasema: "Hivi sasa tunafanya miradi yenye uvumbuzi kwa kulingana na hali mpya ya China, kutoa msaada wa lishe kwa watoto wachanga kwenye maeneo yenye matatizo ya kiuchumi, na kuwasaidia wakulima kwenye sehemu hizo kuongeza mapato na uzalishaji. Pia tutajulisha uzoefu mzuri wa China kwa nchi nyingine zinazoendelea kupitia ushirikiano kati ya Kusini na Kusini."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako