• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Bondia Hassan Mwakinyo kuzichapa na Jose Carlos Paz wa Argentina

  (GMT+08:00) 2020-10-16 17:03:12

  Bondia bingwa wa mabara wa uzito wa superwelter, Hassan Mwakinyo atautetea mkanda wake wa Chama cha WBF Novemba 13 dhidi ya bondia wa Argentina Jose Carlos Paz. Pambano hilo lililopewa jina la 'Dar Fight Night' limeandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports. Mbali ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara wa uzito huo huo wa Chama cha IBA. Pambano hilo limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Next Door Arena.

  Mkurugenzi wa The Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema siku hiyo mabondia kutoka nchi tano watazichapa kumsindikiza Mwakinyo na Paz, akiwamo aliyekuwa bingwa wa dunia wa WBC, Fatuma Zarika kutoka Kenya. Twisa amesema kuwa Zarika atazichapa na Patience Mastara wa Zimbabwe, na Zulfa Yusuph Macho atapambana na Alice Mbewe wa Zimbabwe. Pia siku hiyo, bondia Abdallah Pazi maarufu kwa jina la Dullah Mbabe atacheza na Alex Kabangu wa DR Congo. Alisema kuwa wameamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi kutokana na kutambua vipaji vya mabondia mbalimbali hasa Mwakinyo ambaye anafanya vizuri katika mapambano yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako