Mkurugenzi wa Shirika la fedha duniani IMF Bibi Kristalina Georgieva jana alisema, kutokana na China kuchukua hatua zenye nguvu za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona na kuunga mkono ustawi wa uchumi, uchumi wake utaongezeka na kuwa nguvu za kusukuma mbele uchumi wa dunia.
Bibi Georgieva amesema, ripoti ya makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia ya IMF imeinua makadirio kwa ongezeko la uchumi wa China, sababu ni kwamba China imechukua hatua zenye ufanisi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, na kutekeleza sera za kifedha za kuunga mkono ufufukaji wa uchumi.
Amesema China pia inashiriki kwenye utafiti wa chanjo ya virusi vya Corona, hii itasaidia kuongeza imani ya dunia nzima ya kushinda virusi hivyo, kwani kuinua imani ni muhimu katika kipindi hiki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |