• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kupanua maslahi ya pamoja katika kufungua mlango na kunufaishana fursa katika ushirikiano

  (GMT+08:00) 2020-10-16 20:13:21

  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, China itaendelea kushikilia mkakati wa kunufaishana wa kufungua mlango, kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kupanua maslahi ya pamoja katika kufungua mlango na kutimiza kunufaishana fursa katika ushirikiano.

  Maonyesho ya 128 ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China yamefunguliwa jana. Bw. Zhao Lijian amesema hadi sasa makampuni elfu 26 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 200 yameshiriki kwenye maonyesho hayo.

  Amesema maonyesho hayo ni jukwaa muhimu kwa China kufungua mlango na kufanya biashara ya kimataifa, yamefanyika kwa miaka 63 mfululizo, na kuhimiza kwa nguvu kubwa ushirikiano na maingiliano ya uchumi kati ya China na nchi za nje na maendeleo ya uchumi wa dunia.

  Amesema China haitasimamisha mageuzi na kufungua mlango, na itaendelea kupanua kufungua mlango. China itashirikiana na nchi mbalimbali duniani kupanua maslahi ya pamoja katika kufungua mlango na kutimiza kunufaishana fursa katika ushirikiano, kuhimiza kujenga uchumi wa dunia wa kufungua mlango na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako