• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa afya wa Afrika Kusini aambukizwa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-19 08:58:48

    Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Bw. Zweli Mkhize jana alitoa taarifa akithibitisha kuwa, yeye na mke wake wameambukizwa virusi vya Corona.

    Bw. Mkhize amesema hivi sasa yeye na mke wake wamejiweka karantini nyumbani, lakini hakudokeza namna alivyoambukizwa virusi hivyo.

    Bw. Mkhize amewataka watu waliokutana naye katika siku kadhaa zilizopita kujiweka karantini, vilevile amewahimiza wananchi wa Afrika Kusini waendelee kufuata kanuni husika dhidi ya COVID-19, kuvaa barakoa kwenye maeneo ya umma, na kudumisha umbali wa kijamii pamoja na kunawa mikono mara kwa mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako