Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa ikitangaza kuondoa marufuku ya kusafirisha silaha bila masharti yoyote ambayo iliwekwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.Taarifa hiyo imesema, makubaliano ya suala la nyuklia la Iran yamesema kuwa, kuondoa marufuku dhidi ya Iran kusafirisha na kuingiza silaha hakutahitaji kupitisha makubaliano yoyote mapya au Baraza la Usalama la Umoja huo kutoa taarifa au kuchukua hauta fulani.
Pia imesema, kwa mujibu wa mahitaji ya kujilinda, Iran inaweza kununua silaha na vifaa vyovyote vinavyohitajika kutoka mahali popote bila ya vizuizi vya sheria yoyote na kuweza kuuza silaha za kujilinda kwa mujibu wa sera yake ya kuuza nje.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |